August 3, 2015

MALINZI NA TENGA 

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemshukuru Rais wa CECAFA, Leodegar Tenga kwa kuipa Tanzania uenyeji wa mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) iliyomalizika jana kwa timu ya Azam FC kutawazwa Mabingwa wapya.


Aidha, Malinzi ameishukuru Kamati ya Ndani ya Uendeshaji ya Michuano hiyo (LOC) kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuandaa na kuhakikisha michuano hiyo inafanyika na kumalizika katika hali ya usalama na amani.

Malinzi pia amewapongeza wapenzi, washabiki na wadau wa soka nchini waliojitokeza kushuhudia michezo ya michuano hiyo na kuonyesha nidhamu ya hali ya juu ndani nan je ya uwanja kipindi chote cha michuano.

Rais Malinzi ameipongeza klabu ya Azam FC kwa kutwaa Ubingwa Kagame, kwa kutwaa ubingwa huo imeweza kuweka historia ya kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake na pia kuwa klabu iliyocheza michuano hiyo na kuwa bingwa bila kuruhusu nyavu zake kutikisika.

Pia Malinzi amewashukuru waandishi wa habari/vyombo vya habari kwa sapoti yao wakati wa michuano hiyo. Shukrani hizo pia zimepelekwa kwa klabu za Yanga SC, KMKM kwa kushiriki mashindano hayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic