Na Aidan Mlimila
Mwishoni mwa miaka ya 80 na mwanzoni
mwa miaka ya 2000 ulipokuwa ukitaja Liverpool Fc basi ulikuwa unataja timu
yenye mafanikio kuliko timu nyingine yeyote katika soka la Uingereza ukiachilia
mbali mafanikio waliyokuwa wameyapata kwenye soka la ulaya kwa ujumla kwa maana
ya mashindano yanayoandaliwa na chama cha soka cha ulaya Uefa.
Kwa upande mwingine Liverpool ilikuwa
ndiyo timu ambayo ilikuwa imetwaa mataji mengi ya ligi kuu ya Uingereza kabla
rekodi yao haijavunjwa na mahasimu wao wakubwa katika soka la Uingereza klabu
ya Manchester United ambayo imetwaa mataji 20 mpaka sasa mataji mawili zaidi ya
Liverpool.
Ni muda mrefu sasa Liverpool imekuwa
haifanyi vizuri kwenye ligi kuu ya Uingereza siyo kutwaa Ubingwa tu, bali hata
uhakika wa kumaliza ndani ya timu nne za juu katika ligi kuu ya Uingereza
limekuwa ni tatizo sana kwao kwa misimu mingi ya karibuni.
Tangu Brendan Rodgers alipoteuliwa
kuifundisha Liverpool mwaka 2012 akitokea klabu ya Swansea moja ya kitu ambacho
amefanikiwa kwa kiasi fulani ni kuiwezesha Liverpool kumaliza ndani ya timu nne
za juu msimu wa 2013/14 kitu ambacho watu wa Liverpool walikuwa wamekimisi
kwa muda na ilibakia kidogo msimu huo watwae ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza
kama isingekuwa makosa ambayo waliyafanya na kupelekea kukosa ubingwa dakika za
mwisho.
Kabla ligi haijaanza Liverpool
ilikuwa ni timu ambayo sikuipa nafasi kubwa sana ya kufanya vizuri msimu
huu. Lakini baada ya mechi hizi mbili taratibu naona wameanza kunishawishi na
kunifanya nianze kubadili mtazamo wangu juu yao. Ingawa ni mapema sana
kuzungumzia nafasi ya timu kwa kutumia mechi mbili tu kati ya mechi 38 ambazo kila
timu inatakiwa kucheza msimu mzima.
Lakini ndani ya mechi hizi mbili
ambazo Liverpool wameshacheza mpaka sasa kuna kitu nimekiona ambacho nadhani
kama wataendelea na mwendelezo huu basi wanaweza kuwa ndo ambayo itawashangaza
wengi mwisho wa msimu (Surprise of the Season).
Kwenye idara ya ulinzi Liverpool
mpaka sasa ndani ya dakika 180 hawajaruhusu nyavu zao kuguswa. Na kama
inavyojulikana ili timu iweze kufanya vizuri katika ligi lazma kwanza kabisa
iwe na defense imara kitu ambacho Liverpool wameweza kukionesha ndani ya mechi
hizi mbili. Ingawa mtu mwingine anaweza kuhoji ubora wa timu ambazo Liverpool
imekutana nazo mpaka sasa lakini binafsi wameweza kunishawishi.
Kitu kingine ambacho kinanifanya
nianze kuipa nafasi Liverpool ni kuanza vibaya kwa timu ambazo zilionekana
kutishia nafasi yao katika nafasi nne za juu (Top Four). Arsenal na Chelsea
zimeonekana kutokuwa na mwanzo mzuri mpaka sasa Chelsea wako nyuma ya Liverpool
kwa point tano huku Arsenal wakiwa nyuma kwa point tatu hii ni faida kubwa sana
kwao kwa sababu kadri ambavyo wapinzani wao wanavyozidi kupata matokeo mabaya
ndivyo ambavyo nafasi yao ya kufanya vizuri inapozidi kuongezeka.
Lakini pia ingizo la wachezaji kama
Klyne, Benteke, na Firminio kwa kiasi kikubwa umeongeza kitu kwenye kikosi cha
majogoo hao wa Merseyside. Unapokuwa na mtu kama Benteke kwenye eneo la
ushambuliaji hii ina maana una mtu ambaye ana uwezo wa kukupa siyo pungufu ya
magoli 20 kwa msimu na hii ni kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao wa kufunga
magoli lakini pia kucheza na watu kama Courtinho na Firminio ambao wana uwezo
mkubwa wa kutengeneza nafasi za magoli kitu ambacho kitakuwa faida kwa Benteke
kumfanya afunge magoli mengi ambayo mwisho wa siku yataisadia Liverpool
kukusanya point za kutosha.
Ujio wa Nathaniel Clyne pia umeongeza
kitu kikubwa sana kwenye safu ya ulinzi ya Liverpool. Uwezo wake mkubwa
aliokuwa nao wa kukaba pale ambapo timu inashambuliwa na uwezo wa kusukuma
mashambulizi pale ambapo timu inapokuwa inashambulia bila shaka utakuwa msaada
mkubwa sana kwao.
Kitu kingine ambacho Klyne ataongeza ni uwezo wake mkubwa wa
kupiga krosi kitu ambacho kitaipa Liverpool option nyingine ya kutengeneza
nafasi kupitia kwenye flanks kitu kitakachokuwa faida kubwa pia kwa Christian
Benteke ambaye pia ni mzuri sana hewani (aerial balls).
Na
hapo ndipo Liverpool wanapoanza kunishawishi na kuanza kubadili mtazamo wangu
juu yao
0 COMMENTS:
Post a Comment