August 19, 2015

MOHAMMED HUSSEIN DAIMA WA GLOBAL FC AKIPAMBANA NA BEKI WA DAR CITY.
Timu ya soka ya Global FC imeonyesha soka safi na la kuvutia katika mechi dhidi ya Dar City iliyokuwa inaongozwa na wachezaji wengi vijana wakiwemo wanaocheza timu ya Simba B na timu mbalimbali za Ligi kuu.


Mechi hiyo ya kirafiki kwenye Uwanja wa Ustawi ilizua tafrani baada ya mwamuzi kuacha kwa makusudi na mwamuzi kuruhusu bao ambalo lilionekana ni wazi na baada ya hapo alimaliza mpira na kuondoka zake haraka uwanjani hapo.



CLEMENT KAHABUKA (KULIA) AKIDHIBITI MPIRA MBELE YA SALEH ALLY 'JEMBE' WA GLOBAL FC.

Hata hivyo kiungo cha Saleh Ally, safu ya ushambulizi ya washambuliaji wakongwe wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Mohammed Hussein Daima ‘Chinga One na Edibily Lunyamila ambao ni wachambuzi wa gazeti la Championi pia Ally Mbetu iliwapa wakati mgumu wachezaji vijana wa Dar City.
 
MASHABIKI WAKIWA VIP



Beki ya Bakali malima ‘Jembe Ulaya’ na Sweetbert Lukonge ilizuia washambuliaji wa Dar City waliiongozwa na Athumani Tippo maarufu kama Zizzou au mwili nyumba kufanya lolote.


Mechi hiyo ilikuwa kivutio zaidi kwani wachezaji wa Global FC wengi walikuwa na umri mkubwa huku wale makinda wa Dar City wakionyesha kuzidiwa nguvu na ujuzi.

KIKOSI CHA DAR CITY..


SALEH ALLY 'JEMBE' AKICHANJA MBUGA...



GLOBAL FC...

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic