Mchezo wa Ngao ya Hisani ambao ni sehemu ya ufunguzi wa pazi la
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) nchini kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC utachezwa
siku ya jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salam, ambapo kiingilio
cha chini kitakua ni silingi elfu saba..
Tiketi
za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya mchezo jumamosi asubuhi saa 2 kamili
katika viunga vya maeneo ya uwanja wa Taifa jijini Dar es slaam.
Mchezo
huo wa Ngao ya Jamii utachezeshwa na mwamuzi Israel Mjuni Nkongo, (Dsm),
akisaidiwa na Samwel Hudson Mpenzu (Arusha), Josephat Daud Bulali (Tanga),
mwamuzi wa akiba Hashim Abdallah (Dsm) wakati kamisaa wa mchezo huo ni
Deogratius Rwechungura kutoka mkoani Mara.
0 COMMENTS:
Post a Comment