Manchester City
imemaliza mechi yake ya mwisho ya maandalizi ya msimu mpya kwa kukutana na
kipigo cha mabao 4-2 kutoka kwa wenyeji wake Stuttgart ya Ujerumani.
Katika mechi hiyo
iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mercedes Benz Arena vijana wa Manuel Pellegrini
wakiwa na mastaa wao kama Raheem Sterling, David Silva na Vincent Kompany
lakini hawakuweza kufua dafu dhidi ya kikosi hicho ndani Bundesliga.
Filip Kostic, Daniel
Didavi na mabao mawili ya Daniel Ginczek ndiyo waliofunga mabao hayo manne huku
City wakifunga kupitia Kelechi Iheanacho na Edin Dzeko.
0 COMMENTS:
Post a Comment