Kocha mkongwe katika ukanda wa Afrika
Mashariki, Jacob Ghost Mulee amesema beki wa Azam FC, Serge Wawa kama asingekuwa
mwanasoka, basi alipaswa kuwa mwanajeshi.
Mulee ambaye ni raia wa Kenya na
mchambuzi katika runinga ya SuperSport ameonyesha kuvutiwa sana na Wawa.
“Utaona anavyoiongoza safu yake ya
ulinzi, inaonyesha wazi ni mtu anayeijua kazi yake.
“Si mwoga, akiingia anaingia kweli.
Anacheza kama beki mahiri anavyotakiwa.
“Lakini anaweza kusaidia kupandisha
mashambulizi ya kikosi chake. Naona kama asingekuwa mwanasoka, basi alipaswa
kuwa mwanajeshi,” alisema Mulee.
Wawa ameiongoza safu ya ulinzi ya Azam
FC kutofungwa hata bao moja hadi inaingia fainali ya michuano ya Kagame
itakayochezwa kesho.
Mechi hiyo kati ya Azam FC na Gor Mahia
inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki huku Azam ikiwa haijafungwa hata bao
moja na timu hiyo ya Kenya iliyofungwa mabao 6, lakini haijapoteza hata mechi
moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment