August 23, 2015

MGETA (KULIA) KATIKA TANGAZO LA MECHI HIYO KABLA HAIJACHEZWA.

Timu ya daraja la tano nchini Ujerumani anayochezea Mtanzania Emily Mgeta imeanza ligi kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Heiningen.


Mgeta ameichezea timu yake hiyo ya Neckarsulmer dakika 70 ikiwa ni mara yake ya kwanza kucheza Ligi ya Ujerumani inayotambulika kama Verbandsliga.

Kikosi hicho cha Neckarsulmer kilikuwa ugenini lakini kilifanikiwa kufunga bao kila kipindi.

"Tumeshinda kwa mabao mawili, umekuwa ni mwanzo mzuri ingawa katika dakika ya 70 nilitolewa," alisema.

"Tumecheza vizuri kabisa tena tukiwa ugenini, sasa tunarudi kujiandaa na mechi ijayo," alisema beki huyo wa zamani wa Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic