MALINZI AKIWA NA RAIS WA CAF, ISSA HAYATOU |
Klabu kongwe ya Afrika Kusini, Orlando Pirates, inatarajiwa kuchukua wachezaji
watano chini ya umri wa miaka 15 ambao wanakwenda kwenye majaribio klabuni hapo
na iwapo watafaulu, itakuwa tiketi ya kuchukuliwa moja kwa moja.
Vijana hao wanatarajiwa kuondoka nchini Agosti
29, mwaka huu chini ya Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi ambapo mtihani
wao wa kwanza utakuwa Septemba 5, kutakuwa na mashindano ya Multichoice nao
watashiriki.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal
Malinzi, ametoa shukrani zake kwa Mwenyekiti wa Pirates, Dk Irvin Khoza ambaye
alikuwa mwepesi kukubaliana na ombi lake la kuchukua vijana hao, ikiwa ni
sehemu ya kupanua soko la soka la Tanzania.
Wachezaji hao ni Asad Juma kutoka Zanzibar, Issa
Abdi na Maziku Amad (Dodoma), Athuman Maulid (Kigoma) na Kelvin Deogratius wa
Geita.
Wakati huohuo, jumla ya wachezaji 20
waliochaguliwa kwenye mashindano ya vijana ya taifa yaliyofanyikia Mwanza hivi
karibuni, wanatarajiwa kujiunga na Akademi ya Alliance ya Mwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment