August 23, 2015


Mshambuliaji mpya wa Royal Eagles, Uhuru Selemani ameikosa mechi ya kwanza ya ligi huku timu yake ikitoka sare ya bao 1-1.

Royal Eagles ya jijini Durban imetoka sare hiyo ya bao 1-1 na Highland Park.

Hata hivyo Uhuru alikuwa jukwaani akishuhudia kutokana na kutokuwa na kibali cha kazi.

"Kweli sijacheza mechi hiyo, bado sijapata kibali cha kazi hapa Afrika Kusini. Lakini uongozi umekuwa ukishughulikia.

"Sina uhakika lini kitakuwa tayari ila nimeelezwa kabla ya mechi ijayo huenda mambo yatakuwa poa," alisema Uhuru aliyewahi kuzichezea Simba na Coastal Union.

Uhuru ambaye ni mchezaji wa Jomo Cosmos amepelekwa kwa mkopo katika kikosi hicho cha Royal Eagles kinachomtegemea kukivusha.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic