Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
(TFF) kilichokutana leo kimepitia na kutoa maamuzi yafuatayo:
(i) Kila mkoa utakua na kituo cha kukuza na
kuendeleza vipaji vya watoto (Regional Sports Centre). Mapato ya mchezo wa Ngao
ya Hisani msimu huu yatatumika kuagiza kontena la vifaa (mipira size 3, 4, bips
na cones) ambavyo vitasambazwa katika vituo vyote vya michezo vya mikoa.
(ii) Ubovu wa viwanja – Kamati ya Utendaji
imeiagiza sekretariat kuwaandikia barua wamiliki wa viwanja vyenye mapungufu,
kufanyia kazi marekebisho hayo haraka kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi
nchini. Kiwanja ambacho hakitafanyiwa marekebisho hakitatumika kwa michezo ya
ligi msimu huu.
(iii) Twiga Stars – Timu ya Taifa ya Wanawake
ya mpira wa miguu nchini Tanzania (Twiga Stars) inatarajiwa kuingia kambini
tarehe 04 Agosti kisiwani Zanzibar kwa gharama za TFF kujiandaa na Fainali za
Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofanyika nchini Congo Brazaville
mwezi Septemba mwaka huu. Aidha Kamati ya Utendaji imeiagiza sekretariet
kuwasiliana na Kamati ya Olympic nchini (TOC) kuweza kujua mchango wao katika
maandilizi hayo ya michezo ya Afrika.
(iv) Kamati ya Utendaji imeipongeza Kamati ya
ndani ya Uendeshaji wa Michuano ya Kombe la Kagame (LOC) kwa kuandaa michuano
hiyo vizuri kuanzia mwanzo mpaka sasa inapoelekea mwishoni kesho kwa mchezo wa
Fainali. Aidha Kamati inaipongeza klabu ya Azam FC kwa kufika hatua
ya fainali ya michuano hiyo na kuitakia kila la kheri katika mchezo wa kesho
ili iweze kulibakisha kombe hilo nyumbani. Kamati hiyo pia imeipongeza klabu ya
Yanga kwa kufika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
(v) Aidha Kamati ya utendaji imeiagiza
sekretariat kuandika barua kwenda kwa uongozi wa CECAFA juu ya masikitiko na
mapungufu yaliyoenekana katika michuano hiyo. Timu ya Gor Mahia pamoja na
washabiki wake wamekuwa wakifanya vitendo vya utovu wa nidhamu huku CECAFA
ikiwatazama pasipo kuwapa adhabu yoyote.
(vi) Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji pia
kimepitia na kupitisha mapendekezo ya rasimu ya kanuni za uendeshaji wa Bodi ya
ligi nchini (TPLB), yaliyowasilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria,
Katiba na Hadhi za Wachezaji Wakili, Idd Mandi.
0 COMMENTS:
Post a Comment