Wakati kikosi cha Mwadui FC kikiendelea na maandalizi, kimeendelea
kukumbwa na majeruhi ambao sasa wamefikia kumi na wengi wakiwa kikosi cha
kwanza.
Wachezaji hao ni pamoja na
David Luhende, Athuman Idd ‘Chuji’, Jamal Mnyate, Shaban Kado, Jabir Aziz
‘Stima’, Antony Matogolo, Junior na wengine wengi.
Kocha mkuu wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, alifunguka kuwa,
anaamini wachezaji wake watarejea kwenye afya njema.
“Wachezaji wangu takriban
kumi ni majeruhi lakini ninaendelea na michezo ya kirafiki kwa sababu wapo
wachezaji wengine, japo hakuna anayependa kuumia, siku zote inatokea bahati
mbaya.
“Wengi tayari afya zao zimeanza kuimarika kwa kiasi na wote
wamepata majeraha hayo kipindi hiki cha maandalizi kupitia michezo ya kirafiki,”
alisema Julio ambaye ametangaza kuwa kikosi chake kipo tayari kupigania ubingwa
msimu huu.
Ikumbuke kuwa tayari timu hiyo imecheza michezo saba na timu za
ligi kuu zikiwemo Simba, Azam, Kagera Sugar, Stand United, Toto Africans,
Coastal Union, African Sports, JKT Ruvu na inatarajiwa kucheza na Mtibwa Septemba
6, mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment