August 18, 2015

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajiwa kuondoka nchini siku ya jumamosi usiku kuelekea Muscat Oman, kucheza mchezo wa kirafiki kabla ya kuunganisha kuelekea Istambul Uturuki kwa kambi ya wiki moja.

Taifa Stars imepata mwaliko wa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Oman tarehe 24 Agosti, 2015 usiku, ambapo baada ya mchezo huo timu itasafiri kuelekea nchini Uturuki katika jiji la Istambul.
Shirikisho la Soka Oman (OFA) liliomba kucheza mchezo wa kirafiki na Taifa Star kabla ya kuwavaa Turkemebistan katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia Septemba 03, 2015 kwa bara la Asia, ambapo kocha wake mkuu Mfaransa Paul Leguen aliomba kucheza na vijana wa Charles Boniface Mkwasa kujiandaa na mechi hiyo.
Mara baada ya mchezo huo Taifa Stars itaelekea Istambul katika mji wa Kocael hoteli ya Kartepe kwa kambi ya wiki moja, ikiwa nchini Uturuki Stars inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki kabla ya kurejea nchini kucheza na Nigeria Septemba 05, 2015 mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika.
Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mkwasa anatarajiwa kutoa orodha ya kikosi chake cha wachezaji 22 mwishono mwa wiki watakaosafiri kuelekea nchini Uturuki kwa kambi ya hiyo ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic