Na
Saleh Ally, Kartepe
Kikosi
cha Taifa Stars kimewasili nchini Uturuki tayari kwa kambi ya wiki moja
kujiandaa kuivaa Nigeria.
Stars
imetua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ataturk katika jiji la Istanbul
nchini.
Baada
ya kuwasili Istanbul ilianza safari hadi kwenye mji wa Kartepe ulio juu ya
milima kabisa ambako wataweka kambi yao katika Hoteli kubwa ya kitali ya The
Green Park.
Kumbuka Stars imesafiri kwa saa saba hadi Istanbul kupitia ndege ya Turkish ambayo iliondoka Dar es Salaam saa 9:45 alfajiri na kuwasili saa 4:45 asubuhi.
Taifa
Stars chini ya Kocha Boniface Mkwasa, msaidizi wake, Hemed Morocco, Kocha wa
Makipa, Manyika Peter pamoja na mshauri wa ufundi, Abdallah Kibadeni inatarajia
kuanza mazoezi ya kwanza leo Saa 1 usiku.
Hoteli
hiyo imezungukwa na viwanja vya kisasa kwa ajili ya maandalizi ya timu ambazo
zimekuwa zikiweka kambi hapa.







0 COMMENTS:
Post a Comment