Na
Saleh Ally, Istanbul
Wachezaji
wa Taifa Stars wamepata nafasi ya kuuona uwanja unaomilikiwa na klabu kongwe na
maarufu ya hapa Uturuki ya Galatasaray, huku wengi wakionekana kufurahia.
Galatasaray
inajulikana kutokana na ubora wake pia historia au rekodi nzuri katika michuano
ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wachezaji
wa Stars wakiwa njiani kutoka jijini Istanbul kwenda katika mji mdogo wa
Kartepe walipita karibu na Uwanja wa Turk Telecom Arena ambao unamilikiwa na
Galatasaray.
Kikosi
cha Taifa Stars kimewasili nchini Uturuki tayari kwa kambi ya wiki moja
kujiandaa kuivaa Nigeria.
Baada
ya kuwasili Istanbul ilianza safari hadi kwenye mji wa Kartepe ulio juu ya
milima kabisa ambako wataweka kambi yao katika Hoteli kubwa ya kitali ya The
Green Park.







0 COMMENTS:
Post a Comment