Timu ya taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajiwa kushuka
dimbani siku ya jumapili kucheza dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya (Harambee
Starlets) katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar ukiwa ni mchezo wa kirafiki.
Kocha mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage amesema anaendelea
vizuri na maandalizi, vijana wake wote wapo katika hali nzuri kuelekea katika
mchezo huo wa kirafiki kabla ya safari ya kuelekea nchin Congo-Brazzavile.
Twiga
Stars inatumia mchezo huo wa kirafiki kama sehemu ya maandalizi ya fainali za
Michezo ya Afrika (All Africa Games) zinazofanyika kuanzia Septemba 4-19 nchini
Congo-Brazzavile







0 COMMENTS:
Post a Comment