MGOPE |
Azam TV ambayo itaonyesha moja kwa moja mechi
kati ya watani Simba na Yanga, itafanya mambo special kwa leo.
Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Azam TV, Mgope
Kiwanga amesema wataanza mapema mahojiano mbalimbali kuanzia asubuhi.
Baada ya hapo, mambo yatahamia uwanjani ambako
watani hao watakuwa wakipambana na kusimamisha shughuli zote.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Michezo cha Azam TV,
Baruan Muhuza amesema wanajaua ukubwa wa mechi hiyo ya watani.
“Ni mechi kubwa na mechi ya kihistoria, hivyo
tumefanya hivyo ili kukidhi hamu ya watazamaji wetu,” alisema.
Azam TV ndiyo imekuwa runinga tegemeo
inayoonyesha mechi nyingi moja kwa moja.
Katika sehemu mbalimbali hasa jijini Dar es
Salaam kuna maeneo maalum kwa akili ya kuonyesha mechi hizo kupitia king'amuzi cha Azam TV ambayo sasa ndiyo kubwa zaidi kuliko nyingine zote.
0 COMMENTS:
Post a Comment