Nahodha wa Simba, Mussa Mgosi, leo atacheza
dhidi ya Yanga akiwa na mambo mawili kichwani, moja ni kuipatia ushindi timu
yake, pili kuvunja rekodi ya Abdallah Kibadeni ya kufunga mabao matatu ‘hat
trick’.
Kibadeni alifunga mabao hayo katika dakika za
10, 42 na 89. Mabao mengine ya Simba yalifungwa na Jumanne Hassan ‘Masimenti’
dakika za 60 na 73 na lingine lilikuwa la kujifunga la Selewa Sanga wa Yanga
dakika ya 20.
Mgosi amesema: “Siku
niliyoisubiria imefika, nafikiria kuivunja rekodi ya Kibadeni tu katika mchezo
wa kesho (leo), maana naona miaka inazidi kwenda tu na hakuna anayejitokeza
kuivunja.
“Sisi ndiyo tunatakiwa kuivunja, naamini
nitafanya hivyo katika mchezo huu kutokana na kwamba wachezaji wa Yanga
nawafahamu vizuri tu na hawanipi shida.”
Hata hivyo, tofauti na Hamis Kiiza anayeongoza
kwa ufungaji Simba akiwa na mabao matano na Justice Majabvi mwenye bao moja,
Mgosi ambaye ni straika hajafunga hata bao moja katika mechi mbili za ligi
alizocheza.
0 COMMENTS:
Post a Comment