CANNAVARO |
Mambo yamekucha sasa, kwani nahodha na beki wa
kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema wala hatahangaika kumzuia Hamis
Kiiza wa Simba, badala yake kazi hiyo ataifanya, Mzimbabwe Thabani Kamusoko.
Cannavaro amewahi kucheza pamoja na Kiiza
katika kikosi cha Yanga kabla ya straika huyo kutemwa Desemba, mwaka jana na
sasa yupo Simba.
Tangu alipotua Simba, Kiiza ameonekana lulu
ambapo hadi sasa amefunga mabao matano katika mechi tatu za Ligi Kuu Bara. Leo
Kiiza anaichezea Simba dhidi ya Yanga ikiwa ni mara yake ya kwanza kuivaa Yanga
tangu alipoachwa.
Cannavaro alisema binafsi anamuona Kiiza kuwa
mchezaji wa kawaida kwani anamjua uzuri na ubovu wake awapo uwanjani, lakini
kwa maelekezo kuhusu mchezo huu, Kamusoko ndiye atakuwa anamzuia straika huyo.
“Nimesikia taarifa za Kiiza za kutamba kuwa
atatufunga, lakini ninachomwambia ni kwamba hatapata nafasi hiyo kutokana na
mikakati tuliyoipanga kwa kuanzia kwa mabeki na viungo.
“Huyo nimemkabidhi Kamusoko atembee naye popote
atakapokuwepo na mimi pamoja na Yondani (Kelvin) tumechukua majukumu mengine ya
kumdhibiti mwingine atakayecheza na Kiiza, sisi hawezi kutusumbua kwani
tunamjua vizuri tu,” alisema Cannavaro.
KIIZA (KULIA)... |
Alipoulizwa kuhusu mkakati huo
wa Yanga, Kiiza alicheka kidogo kisha akajibu: “Hiyo hainiogopeshi, badala yake
kama mshambuliaji nitatimiza wajibu wangu wa kufunga kwa kila nafasi
nitakayoipata.”
SOURCE: CHAMPIONI JUMAMOSI
0 COMMENTS:
Post a Comment