September 25, 2015


Straika wa Yanga, Malimi Busungu, juzi Jumatano katika mazoezi ya timu hiyo iliyopo kisiwani Pemba alitoa kali ya mwaka baada ya kumvaa kocha wake mkuu raia wa Uholanzi, Hans van Der Pluijm akimtaka ampatie dakika 30 tu kwenye mchezo wa kesho Jumamosi wa Ligi Kuu Bara ili aivuruge Simba.


Busungu, straika aliyetua akitokea Mgambo ya Tanga, mwanzoni mwa msimu huu, amejikuta akiwa chaguo la tatu la Pluijm nyuma ya Amissi Tambwe na Donald Ngoma, alifikia hatua hiyo baada ya kudai kuwa ana bahati ya kuifunga Simba kila anapokutana nayo.

Busungu amesema tangu alipoanza kukutana na Simba, amekuwa akiifunga, hivyo anaamini endapo Pluijm atakubali ombi lake hilo la kumpatia dakika 30 kwenye mchezo huo, basi atawavuruga vibaya Simba kwa kuzifumania nyavu zao kwa zaidi ya mara moja.

“Najiamini kuwa naweza kufanya hivyo endapo nitapewa nafasi kwani ukuta wa Simba jinsi ulivyo hakika hakuna beki wa kunisumbua nisifanye yangu,” alisema Busungu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic