Kocha Mkuu wa Majimaji ya Songea, Mika Lonnstrom
raia wa Finland amesema vitendo alivyokutana navyo kwenye mchezo uliopita dhidi
ya JKT Mgambo, bado vinamsumbua akili kwani anashangaa kwa nini vimetokea
kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Wiki iliyopita, Kocha Mkuu wa Toto African, John
Tegete alilalama kupulizwa kwa dawa kwenye vyumba vyao vya kubadilishia nguo
wakati walipocheza na Coastal Union. Lakini meneja wa Uwanja wa Mkwakwani
akadai walipulizia manukato tu.
Majimaji wamekuwa wakilalamika kuwa walipuliziwa
hewa yenye sumu katika vyumba vyao vya kubadilishia nguo wakati timu hizo
zilipokutana kwenye Uwanja wa Mkwakwani, wiki iliyopita hali iliyowafanya
waambulie kipigo cha bao 1-0.
Kocha huyo ameliambia gazeti hili kuwa alikuwa hajui
kama Tanzania kunaweza kuwa na fitina za soka kiasi hicho, kwa kuwa amebaki na
mshangao mkubwa kiasi cha kukosa majibu juu ya kile alichokishuhudia.
“Nimeshtushwa sana na hali ile, kama ligi ndiyo
iko hivi, kwa kweli ni jambo la kushangaza, inapaswa TFF wawe wakali kwa kuzipa
adhabu kali timu zinazofanya vitendo kama hivi. Lakini nimejifunza,” alisema
Lonnstrom.
0 COMMENTS:
Post a Comment