![]() |
| KESSY (KULIA) AKIWA NA SSERUNKUMA |
Beki wa kulia wa Simba, Hassan Kessy, tayari
amejiandaa kuikabili Yanga leo huku akiwa na staili mpya ya mtindo wa nywele
ambayo ni maalum kwa mechi ya leo tu.
Simba na Yanga zitapambana kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam katika muendelezo wa Ligi Kuu Bara. Timu zote
zilikuwa kambini visiwani Zanzibar ambapo Yanga ilikuwa Pemba na Simba Unguja.
Kessy amenyoa mtindo unaofanana na kiduku ambao
huondoa nywele za pembeni ya kichwa na kubakiza za katikati kuanzia mbele ya
kichwa hadi nyuma.
Katika mtindo huo mpya, Kessy amenyoa nywele
zote na kuzibakisha kidogo katikati ya kichwa.
Mtindo huu unamfanya Kessy aonekane tofauti
kidogo awapo uwanjani na alipoulizwa sababu ya kunyoa hivyo alisema: “Kinyozi
wangu ndiye aliyeniambia ninyoe hivi ili nionekane tofauti katika mchezo huu.”








0 COMMENTS:
Post a Comment