Na Haji Manara
Kitaaluma
mm si kocha ingawa nilibahatika kupata mafunzo ya awali ya ukocha wa kandanda
ambayo hainiongezei lolote kwenye taaluma hyo nzito.
Nimeangalia vizuri game yetu tena kwa
jicho maalum la fikra chanya. Kwanza niwapongeze sana wachezaji wetu kwa kiwango chao, wamejitahidi sana. Nasema kiwango chao kwa sababu kisoka Nigeria ni mbingu
na ardhi na sisi.
Bofu na pofu!
Mbuzi na swala!!
Kimsingi wamejituma sana leo na ndio
silaha yao, ushindi wa sare leo ni kutokana na kujituma kuliko pitiliza toka kwa
wapiganaji wetu wa Stars.
Yaan kujituma kwa Stars leo
ukichanganya na uwezo wa Mbwana Samatta uwanjani kulikuwa zaid ya burudani pale Uwanja wa Taifa.
Kwangu Samatta ni mchezaji bora sana
ambaye siamini bado analikata pori la DR Congo hata kama tajiri Moise Katumbi anaendelea
kumwaga faranga kwake.
Tuna uhaba mkubwa wa wachezaji wenye
maamuzi bnafsi (si vipaji), bnafsi ni maamuzi ya kufanya jambo kwa ajili ya timu.
Kuamua kuchukua kijiji na
kukisongesha mbele ni Samatta tu Tanzania kwa sasa!!
Ulimwengu pia ni mfano wa maamuzi
hayo ingawa huathiriwa na uwezo wakati mwingine!
Ukijumlisha na kikosi chenye, ngoja
nidadavue maksi kwa mtazamo wangu kabla sijaja kwa wakubwa wa mpira.
Ally mustafa7√10
Utulivu ni silaha ya golikipa huyu
mpole na mchamungu
Shomari kapombe5√10
Kapombe bado hajarudi kwenye ubora
wake kabla hajaenda Ufaransa. Anafanya makosa mengi na amepoteza kujiamini kwake
Haji Mwinyi7√10
Wajina wangu aliniangusha first
half.ila kipindi cha pili baada ya Sunday Oliseh kubadilisha mfumo alisaidia
sana kusuma mashambulizi.ingawa yupo dhaifu kwenye marking ya man to man
Nadir Haroub 'Cannavaro' 8√10
Kwangu legend huyu wa Yanga ni
kisiki kamilii. Mipira yote ya juu alwayz ni chakula chake, ingawa speed yake imepungua mno. Lakini kwa mabeki tulionao, yeye bado anastahili kuendelea kuwa
libero wa nchi
Kelvin yondani5√10
Uwepo wa Cannavaro na kutokuwa sharp
kwa washambulizi wa kipopo ndio salama yake na yetu.
Mipira yote ya one against one
kaachwa.
Rafu zisizo na tija.shukran refa kwa
kumlinda stoper huyu.
Himid Mao mkami6√10
Neno pekee nnaloweza kusema kuhusu
mido huyu ni mkabaji eneo sahihi wakati wote. Ila kwenye passes kaniangusha, kwani si ndefu wala fupi ingawa bado umri mdogo unamlinda.
Farid Mussa8√10
Nilianza kumfaidi kwenye Kagame, ni
tunda linalosubiri kuliwa na taifa hili. Speed na ball control yake
utaipenda, nna hakika akipata uzoefu tutakuwa na mchezaji wa level ya juu ingawa
second half alikuwa taaaban.
Mrisho ngasa7√10
Anko anaweza asikupe maamuzi sahihi
unapomtizamia ila kwa aina ya mifumo yetu na style yake anastahili kuendelea
kutupa mbio zake ila yeye ndio aliokosa bao la wazi zaidi na pia anko always
huchelewa kutoa pasi wakati mwafaka.
Thomas Ulimwengu 9√10
Ni bull wa nchi kama tungekuwa na
timu iliokamilika huyu ni old school striker ni kama gard muller au JJ Masiga.
Hebu pakini mabegi yenu kule
Lubumbashi
Mudathir Yahya 7√10
Dynamo midfielder, msumbufu ingawa
hukosa utulivu kwenye passes, ila ni mkabaji hasa na aliwachosha viungo wa
Nigeria kwa tackling zake.
Mbwana Samatta 10√10
Ningekuwa nacheza leo mpira
ningependa kucheza na huyu pele wa nchi kwa sasa .
Vyovyote usemavyo ndio nyota wa
mechi ya leo.
SUB
Said Ndemla 9√10
Kwangu mimi sina la kusema kuhusu Ndemla ni samli kwenye
mkate wa kusukuma. Ni computer wa kizazi cha sasa.
Akiongeza nguvu nnamuona angani
kwenda kusukuma soka nje
Simon Msuva 6√10
Hakupata muda mrefu wa
kucheza.ingawa pia hakuwa mbaya lakini bad luck, dogo papara zinakuwa
zinamharibia.
John bocco 7√10
Ni mchezaji halisi wa kizazi hiki
cha timu ya taifa.
Sijawahi kumuelewa ingawa inaonekana
anapenda taifa lake.
Na lazma niwe mkweli umbile lake
refu kwa mabeki ni hofu kwao na leo aliingia kipindi ambacho Ndemla alikuwa
anadarsisha na yeye kung`ara pia.
0 COMMENTS:
Post a Comment