June 9, 2020


SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) limeupiga pini Uwanja wa Simba Mo Arena kwa matumizi ya mechi za kirafiki.

Jana, Juni 7 Uwanja huo ulitumika kwa mechi ya kirafiki kati ya Simba na KMC ambapo Simba ilishinda mabao 3-1.

TFF imesema kuwa uwanja huo utatumika kwa ajili ya mazoezi na sio mechi za ushindani.

Sababu kubwa ni kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona na kuzitaka timu zitakapoandaa mechi kuzingatia muongozo uliotolewa na Serikali.

7 COMMENTS:

  1. Kwani mkiwambia kwa kuwapa onyo haifai lazima wafungiwe basi hata mazoezi wafungieni wakachezee uhuru ama kwa mchina ili mradi mpate mapato tu kwa sababu hao kandambili aka GONGOWAZI hawana kiwanja?

    ReplyDelete
  2. Chukuweni na kiwanja sisi ndio mabingwa mara 3 mfululizo na bado mara 2 tena tuwe mara 5 mfulilizo GONGOWAZI aka kandambili watapata tabu sana

    ReplyDelete
  3. TFF mnadumaza mpira wa miguu. Hatuwezi tena kuiogopa corona lililo muhimu ni kuchukua tahadhari. Waelekezeni nini wafanye kuchukua tahadhari lakini sio kuwakataza mechi za kirafiki. Hivi hamuoni fahari timu nyingi kujitegemea viwanja? Corona ipo tutaendelea kuishi nayo ina maana timu zote zitacheza mechi zao za kirafiki viwanja vya Uhuru na Mkapa tu?

    ReplyDelete
  4. TFF mnadumaza mpira wa miguu. Hatuwezi tena kuiogopa corona lililo muhimu ni kuchukua tahadhari. Waelekezeni nini wafanye kuchukua tahadhari lakini sio kuwakataza mechi za kirafiki. Hivi hamuoni fahari timu nyingi kujitegemea viwanja? Corona ipo tutaendelea kuishi nayo ina maana timu zote zitacheza mechi zao za kirafiki viwanja vya Uhuru na Mkapa tu?

    ReplyDelete
  5. Gongowazi kimya, wanasema wanamngojea Mnyama kutokana na uwezo wao mkubwa waliouonesha kwa KMC

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic