Kocha Mkuu wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr,
ameonekana kutokuwa na wasiwasi kabisa na mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya
Yanga kwa jinsi anavyowafanyisha mazoezi wachezaji wake.
Katika mazoezi ya Simba yaliyofanyika jana
asubuhi kwenye Uwanja wa Amaan visiwani hapa, kocha huyo muda wote alionekana
mtu mwenye furaha kwa wachezaji wake, tofauti na makocha wengine wanapokuwa
kwenye maandalizi ya mechi kubwa kama hiyo, hali ambayo inaonyesha wazi ana
uhakika kuwa kile anachokielekeza kinafanyiwa kazi.
Licha ya hayo yote, lakini kocha huyo ambaye ni
rafiki wa kila mtu, alikuwa akiwapa moyo wachezaji wake pindi wanapokosea
maelekezo yake kwa nia ya kutowakatisha tamaa na kuwatoa mchezoni kuelekea
mechi hiyo ambayo ina presha ya hali ya juu.
Kwa upande wa wachezaji, nao walikuwa ni wenye
furaha muda wote na kujisahaulisha kabisa mechi hiyo kwani hakuna hata mmoja
aliyekuwa akionekana mwenye kuifikiria kwa jinsi walivyokuwa wakionekana.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment