Kama akitamka maneno haya mbele ya mashabiki wa
Simba na Yanga, basi anaweza kuingia katika wakati mgumu.
Ofisa Habari wa Ruvu Shooting ya Daraja la
Kwanza, Masau Bwire amesema mastraika Hamis Kiiza wa Simba na Donald Ngoma wa
Yanga hawatafanya lolote katika mchezo wa leo.
Wakati leo Jumamosi Ruvu Shooting ikicheza
mechi ya daraja la kwanza dhidi ya Njombe Mji mjini Njombe, Simba na Yanga
zenyewe zinapambana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika Ligi Kuu Bara.
Bwire amesema mara zote mechi za Simba na Yanga
hukosa ufundi hivyo ni ngumu kwa mchezaji nyota kuonyesha uwezo wake halisi,
hivyo Ngoma na Kiiza wataonekana wa kawaida tu.
Kiiza ndiye nyota wa Simba kwa sasa akiongoza
kwa ufungaji kwa mabao matano aliyonayo wakati Ngoma naye anag’ara Yanga akiwa
amefunga mabao matatu sawa na Amissi Tambwe kikosini.
“Siku
zote mechi hii ya watani huwa ya kukamiana na kupoteza hata ladha ya mchezo,
kama kuna mtu anadhani Kiiza au Ngoma mmoja wao atafanya vizuri huyo atakuwa
anakosea.
“Ngoma
na Kiiza wanaonekana wazuri, ushishangae wakapoteana kabisa kutokana na soka la
hovyo litakalochezwa na timu hizi,” alisema Bwire.
0 COMMENTS:
Post a Comment