Na Mohammed Said
Kocha Hans van Der Pluijm amesisitizia
wachezaji wake kucheza mipira ya chini kila wanaposhambulia na mwisho wa
kucheza mipira ya juu ni katikati ya uwanja tu.
Kuanzia katikati kwenda mbele washambuliaji wa
Yanga wameelekezwa kutuliza na kuizima mipira yote ya juu na kuweka chini kisha
kucheza soka la kuonana hadi golini.
Katika mazoezi ya Yanga siku zote kisiwani
hapa, Pluijm ameonekana akiwasisitizia
wachezaji wake kucheza mpira chinichini muda wote na hata krosi zao
nyingi zilikuwa za chini.
Washambuliaji wa Yanga walionekana kuuzoea
mfumo huo jambo lililoonekana kumfurahisha Pluijm na msaidizi wake, Charles
Mkwasa.
Katika mazoezi ya juzi, viungo na washambuliaji
wa Yanga walionekana kucheza kwa ufasaha mtindo huo anaoutaka kocha wao kiasi
cha kupongezwa kila walipokuwa wakipata bao.
Kwa vyovyote vile, Yanga itautumia mfumo katika
mchezo wake wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment