Mohammed Said, Chake Chake
Mashabiki wa Simba wameyabeza mazoezi ya Yanga
kwa kusema ni ya kawaida na kamwe wasijidanganye kama yatawawezesha kuifunga
timu yao.
Mmoja wa wapenzi wa Simba kisiwani hapa, Ali
Yussuf amesema kuwa, Yanga inayonolewa na Kocha Hans van
Der Pluijm siyo timu ya kuitisha Simba, badala yake wanapaswa kurudisha kwanza
kipigo cha mabao 5-0 walichokipata mwaka 2012.
“Nimetazama mazoezi haya ya Yanga lakini
nakuambia haitaweza kufanya lolote kwa Simba, wana kazi kubwa ya kurudisha zile
bao 5-0 tulizowafunga,” alisema Yussuf.
Shabiki mwingine aliyefahamika kwa jina la
Mbwana Amour, alisema anaamini timu yao ya Simba haipo vizuri lakini amepata
faraja na mazoezi ya Yanga kwani ni ya kawaida sana.
“Kwa mazoezi haya ya Yanga, nadhani hata kama
Simba ipo vibaya kama ilivyo haiwezi kufungwa, ni ya kawaida mno,” alisema
Amour. Yanga iliondoka Pemba, jana Ijumaa kurejea Dar es Salaam tayari kwa
mchezo wa leo dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Tayari Yanga iko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi hiyo ya leo ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment