Na Saleh Ally
Mshambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana Samatta amesema
mechi kubwa za watani kama hii ya leo inayowakutanisha Simba na Yanga, hazina
presha kubwa kwa wachezaji.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Samatta ambaye aliwahi kukipiga Simba, amesema mechi
hiyo zaidi inakuwa na presha kubwa kwa makocha pamoja na mashabiki.
“Utaona wachezaji angalau kidogo wanaweza kutulia na
kufanya vitu vizuri, lakini kwa makocha pamoja mashabiki kunakuwa na presha
kubwa sana,” alisema Samatta mbaye kwa sasa ni kati ya washambuliaji gumzo.
“Tena naona kuna wachezaji wengine hupenda sana kuwa
kwenye vikosi vya mechi hiyo kutokana na ladha tofauti kabisa ukilinganisha na
mechi nyingine.”
Akizungumzia kuhusiuana na ishu ya Simba kuonekana
kutawala pbano hilo la watani huku Yanga ikionekana kushindwa karibu kila
wanapokutana katika miaka hivi karibuni, alisema:
“Nadhani Yanga wanapokea presha zaidi kutokana na
jinsi kila wakati wanapokutana na Simba, kikosi chao kinaonekana kuwa bora zaidi
ya Simba.”
Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili, muda mchache kutoka
sasa na tutakuwa tukiwaletea maendeleo ya uwanjani kwa dakika zote 90.
0 COMMENTS:
Post a Comment