Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema itakuwa ni hatari sana kama waamuzi watakaa kimya uchezaji wa kibabe wenye kulenga kuwaumiza wachezaji wa timu maarufu au kubwa.
Pluijm amesema, wachezaji wa Prisons
walionekana wazi kuzidiwa kiushindani walipocheza nao na walilenga kuumiza
wachezaji wa Yanga.
“Hazikuwa faulo za kimpira, walikuwa
watu waliolenga kuwaumiza wachezaji wangu. Ni kitu kibaya kabisa na haiwezi
kuwa sahihi,” alisema Pluijm.
“Hakuna soka bila faulo, lakini faulo
ya kisoka na faulo iliyo nje ya soka zinatofautiana pia ni vitu vinavyoonekana
wazi.”
Kocha huyo Mholanzi alisema kuna kila
sababu ya waamuzi kukaa chini na kulijadili suala hilo.
Ikiwezekana wachezaji walindwe na kuwe
na adhabu kali kuwakumbusha wale wanaolenga kuumiza wengine kwa makusudi.
Undava wa Prisons huku ikipoteza kwa bao 3-0 dhidi ya Yanga, ulisababisha Pluijm kuzozana na mwamuzi wa mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment