HIKI NDIYO KIKOSI CHA KWANZA CHA YANGA 2015 KUANZA KUCHEZA MECHI YA KWANZA YA LIGI KWA MSIMU WA 2015-16. |
Baada ya kucheza mchezo mmoja dhidi ya Coastal Union ya Tanga jana
Jumapili, Kocha Mkuu wa Yanga, Mdachi Hans van Der Pluijm, ametamka kuwa,
ameandaa mipango madhubuti ya kuhakikisha kikosi hicho kinashinda michezo yake
mitatu iliyobaki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar kabla ya kuanza kuzunguka mikoani
kusaka pointi.
Keshokutwa Jumatano, Yanga itacheza na Tanzania Prisons, kisha JKT
Ruvu kabla ya kucheza na Simba Septemba 26. Pluijm amejipanga kushinda mechi
hizo za Uwanja wa Taifa mapema kabisa kabla ligi haijachanganya.
Pluijm ambaye ni kocha wa zamani wa timu ya Berekum Chelsea ya
Ghana, amesisitiza kuwa ni lazima kikosi
chake kuhakikisha kinaibuka na pointi hizo katika uwanja wa nyumbani ambazo
zitakisaidia katika harakati za kutetea ubingwa.
“Tumeweka mipango ya
kuhakikisha hatupotezi hata mchezo mmoja ambao tutacheza katika Uwanja wa Taifa
katika michezo yetu minne ya awali (ukiwemo wa jana) ambayo tutachezea katika
uwanja huo.
“Pointi hizo ni muhimu kuzipata kwa ajili ya kuweza kutusaidia
katika harakati zetu za kutetea ubingwa ambapo tunawaambia wapinzani wetu
wajiandae vizuri, kwa sababu tunakuja,” alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment