Simba imekuwa ikiendelea na mazoezi yake katika kambi maalumu mjini Zanzibar.
Simba inajiwinda tayari kwa mechi yake dhidi ya watani wake wa jadi Yanga, Jumamosi.
Yanga inakutana na Simba
katika mechi hiyo ya kwanza ya msimu kwa timu hizo kukutana.
Chini ya Kocha Mkuu,
Dylan Kerr, Simba imekuwa ikifanya mazoezi mara mbili kwa siku.
Mazoezi yake yanaonekana
kuwa ni ya mpira zaidi ingawa siku walipotua Zanzibar, mazoezi ya kwanza
walianza na kutafuta stamina.
Tayari Simba imeshinda
mechi zake zote tatu za mwanzo ikianza kwa kuitwanga African Sports bao 1-0,
ikaishindilia Mgambo Shooting 2-0, halafu ikarejea Dar es Salaam na kuituliza
Kagera Sugar 3-0 huku mshambuliaji wake, Hamisi Kiiza aking’ara.
0 COMMENTS:
Post a Comment