Ingawa Kesho Alhamisi ni sikukuu ya Iddi
El Hadji, Yanga wataendelea na mazoezi ya kumuwinda ‘Myama’, Simba.
Yanga ipo kisiwani Pemba kujiandaa na
mechi hiyo dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
Jumamosi.
Ingawa haijajulikana kama watafanya
mazoezi mara mbili, lakini Yanga italazimika kufanya mazoezi siku hiyo ikiwa
siku mbili kabla ya mechi.
Kwa kawaida, Simba itapumzika Ijumaa
siku ambayo inaweza kufanya mazoezi mara moja pia.
Hivyo haitakuwa lahisi kupumzika
Alhamisi na Ijumaa, italazimika kufanya mazoezi kuhakikisha inakuwa vizuri hata
kama haitakuwa siku mbili.
Tokea imefika mjini hapa, Yanga imekuwa
ikifanya mazoezi mara mbili kwa siku kujiandaa na mechi hiyo ya watani wake
ambao tayari wana pointi tisa kama wao.
0 COMMENTS:
Post a Comment