Baada ya kelele nyingi
kutoka kwa wadau wa soka, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema haina
shida watarejesha matumizi ya tiketi za kielektroniki lakini halijui lini
zitaanza kutumika.
Wadau
mbalimbali wa soka kwa muda mrefu wanailaumu TFF kwa kuacha kutumia mfumo wa
tiketi za kielektroniki kuingia katika viwanja vinavyotumiwa kwa mechi za Ligi
Kuu Bara.
Wakati
inasitisha matumizi ya tiketi hizo, TFF ilisema ilikuwa inakumbana na tatizo la
miundo mbinu kutoendana na mfumo wa tiketi hizo ikiwa ni pamoja na uhaba wa
milango katika baadhi ya viwanja.
Katibu
Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, amesema wapo
kwenye mchakato wa kuhakikisha wanaurejesha tena utaratibu huo msimu huu,
lakini bado haijajulikana utaanza lini.
“Tupo
kwenye mchakato wa kutatua zile changamoto zilizojitokeza wakati wa matumizi ya
tiketi za elektroniki, tunapambana kuhakikisha tunaurudisha kwa kuwa sasa
tumesimama kwa muda,” alisema Mwesigwa.
“Siwezi
kusema utaanza lini na katika mechi ipi, lakini ndipo tunakoelekea kwenye msimu
huu ili tuachane na mfumo huu wa sasa.”
Pia
mfumo huo wa tiketi uliokuwa unatumika kwa ushirikiano na Benki ya CRDB,
ulikumbwa na changamoto nyingine ya uchache wa mashine za kuchapa na kuhakiki
tiketi hizo uwanjani.
0 COMMENTS:
Post a Comment