September 19, 2015

FRIENDS RANGERS...

KINDUMBWENDUMBWE cha Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2015/16 kinaanza leo Jumamosi katika baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara huku Ruvu Shooting ya Pwani ikitinga uwanjani kuanza harakati za kurudi ligi kuu.


Katika ligi hiyo msimu huu, timu zimegawanywa katika  makundi matatu tofauti na msimu uliopita ambapo zilikuwa katika makundi mawili tu.

Msimu uliopita timu za daraja la kwanza zilizopanda kwenda Ligi Kuu Bara ni Majimaji na African Sports kutoka Kundi A na Mwadui FC na Toto Africans zikitokea Kundi B.

Ligi hiyo katika msimu mpya itakuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na jinsi timu zilivyofanya maandalizi ya nguvu kuhakikisha zinapanda ligi kuu msimu ujao wa 2016/17.

Makundi yapo matatu na kila moja lina timu nane ambapo timu moja kutoka kila kundi ndiyo itakayopanda daraja ikiwa na pointi nyingi huku yenye pointi pungufu ya wengine itashuka.

KUNDI A
Kundi hili litaundwa na timu za African Lyon FC, Ashanti United SC, Friends Rangers FC, Kiluvya United FC, Kinondoni Municipal Council FC, Mji Mkuu FC, Polisi Dar na Polisi Dodoma.
Katika kundi hili  timu ambazo hazikuwemo msimu uliopita ni Mji Mkuu kutoka Dodoma na Kiluvya United ya Pwani.

KUNDI B
Hili ni kundi lenye changamoto kubwa kwani ipo timu ya Ruvu Shooting iliyoshuka kutoka ligi kuu msimu uliopita. Timu nyingine za Kundi B ni Polisi Moro, Burkina Faso, Njombe Mji FC, Kurugenzi, Lipuli, Kimondo FC na JKT Mlale.
Timu nyingine iliyotoka ligi kuu katika kundi hili ni Polisi Moro, hivyo kazi ipo kwa klabu nyingine kama Kimondo na Lipuli.

Kundi C
Kundi C nalo lina timu nyingi za ushindani kwani uwepo wa JKT Oljoro, Rhino Rangers na Polisi Mara unalifanya liwe kundi la hatari zaidi. Timu nyingine za kundi hili ni Geita Gold SC (Geita), JKT Kanembwa FC (Kigoma), Mbao FC (Mwanza), Panone FC (Kilimanjaro) na Polisi Tabora.

RATIBA:
Leo Jumamosi

KUNDI A
Polisi Dar v Friends Rangers uwanja wa Mabatini

KUNDI B
JKT Mlale v Ruvu Shooting  uwanja wa Majimaji

KUNDI C

Rhino Rangers v Polisi Tabora uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic