NGOMA NA KAMUSOKO.... |
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm
amewapa wachezaji watatu kazi ya kuhakikisha wanapiga mipira ya adhabu ndogo
katika mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Simba.
Mipira hiyo ya adhabu maarufu kama
‘mipira iliyokufa’, itakuwa ikipigwa na kiungo Thabani Kamusoko na
washambuliaji Donald Ngoma na Kamusoko.
Wachezaji hao walifanya kazi ya kupiga
mipira hiyo chini ya mazoezi yaliyoongozwa na Pluijm na msaidizi wake, Charles
Boniface Mkwasa kwenye Uwanja wa Gombani.
Mazoezi hayo yaliyofanyika kuanzia Saa 9
Alasiri hadi Saa 12 jioni kwenye uwanja huo, yalikuwa kivutio kwa mashabiki
walioruhusiwa kuingia uwanjani hapo.
Yanga ipo mjini hapa kujiandaa na mechi
yake hiyo dhidi ya watani na Pluijm alionekana kuwa makini kwa kila jambo
linaendelea huku akisisitiza lifanyike kwa ufasaha.
Tayari Tambwe, Ngoma na Kamusoko, kila
mmoja ameshafunga katika mechi tatu za mwanzo za Ligi Kuu Bara ambazo Yanga
imecheza.
0 COMMENTS:
Post a Comment