RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI AKIWA NA RAIS WA CAF, ISSA HAYATOU |
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) leo hii limeamuru
Kamati ya muda inayoongoza Chama cha Mpira Zanzibar (ZFA) iondoe mahakamani
mashatka yote dhidi ya uongozi halali wa ZFA.
CAF
inaigiza kamati ya muda ya ZFA hadi tarehe 07 Novemba, 2015 iwe imetekeleza
maagizo na kuhakikisha uongozi halali uliochaguliwa na ZFA unarejea katika
shughuli zake uongozi ZFA.
Jambo
hili lisipotekelezwa CAF imesema itaifungia Zanzibar uanachama wake. Kikanuni
na kikatiba kufungiwa uanachama maana yake ni Mwanachama husika kusitishwa
ushiriki katika shughuli zote zinazosimamiwa na FIFA, CAF na wanachama wake
wote.
Shughuli
hizo ni pamoja na kushiriki mashindano ya kimataifa, kozi mbalimbali na misaada
ya kifedha, vifaa, ufundi nk.
TFF
inatoa wito kwa mara nyingine kwa pande zinazokinzana kukaa meza moja na
kumaliza tofauti zao kwa faida ya mpira wa Zanzibar, Tanzania na Ukanda wa
Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
0 COMMENTS:
Post a Comment