Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetuma salamu za pongezi
kwa viongozi wa mpira wa miguu nchini waliochaguliwa kuwa wabunge na madiwani
katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.
Viongozi waliochaguliwa katika nafasi ya Ubunge ni John Kadutu –
mbunge wa Ulyankulu – Tabora, (mjumbe wa mkutano mkuu kutoka Mwanza) na Alex
Gashaza – mbunge wa Ngara (Makamu mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kagera)
Aidha
waliochaguliwa Udiwani katika maeneo yao ni Khalid Abdallah (Mjumbe wa kamati
ya Utendaji – TFF), Yusuph Kitumbo- (Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa
Miguu mkoa wa Tabora), Omari Gindi- (Mwnyekiti wa Chama cha mpira wa Miguu mkoa
wa Kigoma), Bathromeo Kimaro - (Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa
Singida) na Omar Kinyeto (Mjumbe wa mkutano mkuu mkoa wa Singida), Golden
Sanga (Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Ruvuma), Pachal Kihanga
(Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa mkoa Morogoro), Yusuf Manji (Mwenyekiti wa
klabu ya Yanga SC) ambao wote ni wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF.
TFF inawaomba
kutumikia halmashauri zao kwa mafanikio na kutilia mkazo kuhifadhi maeneo ya
wazi kwa ajili ya michezo mbalimbali hususani mpira wa miguu mashuleni.
0 COMMENTS:
Post a Comment