DULLY SYKES |
Na
Saleh Ally
Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Dully Sykes amesema anaamini adhabu
aliyopewa beki Juma Nyosso ya kutocheza miaka miwili ni uonevu.
Dully
ambaye anajulikana na nyimbo zake kama ‘Salome’, Julietha', 'Handsome', 'Bijou', 'Tamika' na ‘Ladie Free’ alizotamba nazo enzi
zake, amesema Nyosso amekosea, hasa kurudia mara ya pili, lakini adhabu hiyo
imekwenda kisiasa na kulenga kumkomoa.
“Sikiliza
ndugu, mnapopambana kila mchezaji anafanya ujanja kuwachanganya wapinzani.
Ikiwezekana anataka kumtengenezea kadi nyekundu mchezaji wa timu pinzani.
“Si
umeona Chelsea kuna kila Diego Costa. Italia Mario Balotelli, pia unamkubuka
Gazza wa England? Wote hao ni vichaa wa soka.
“Hata
katika muziki tuna akina Balotelli, mafano mimi hapa. Pia kuna wachezaji wapole
na wasanii wastaarabu kama akina AY, MwanaFA. Yote haya yapo.
“Nafikiri
kama ni adhabu kutokana na makosa yake, basi wangempa adhabu ya miezi sita
angalau, lakini sio miezi sita.
“Unajua
wanataka kufanya hiyo kupiga (…..) ni kama kitu cha ajabu sana katika soka.
Wakati ni mambo yanaendelea kila siku.
“Mimi
nilikuwa kipa wakati nacheza soka, Nyosso ni beki wangu, nimekua naye pamoja
kule Ilala. Hakuwa mtu wa namna hiyo, lakini najua alikuwa anapambana kwa ajili
ya timu yake,” alisema Dully.
Tayari
Nyosso ameanza kutumikia adhabu hiyo ikiwa ni ya pili baada ya ile kufungiwa
mechi nane baada ya kumtomasa Elius Maguli wakati akiwa Simba, Januari mwaka
huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment