October 16, 2015


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, ameibuka na kuibua hoja kuhusiana na suala la kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’ huku akisema hadi sasa Simba haijapokea barua ya hukumu yake kuwa ni huru kabla hajajiunga na Azam FC.


Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliamua Singano kuwa mchezaji huru na baada ya siku chache akatua Azam FC.

Lakini Hans Poppe amesema hadi jana hawakuwa wamepata barua ya hukumu hiyo kutoka TFF kuhusiana na uamuzi huo.

 “Kweli hadi leo hatuna barua, zaidi ya kusikia na kusoma kwenye vyombo vya habari. Pamoja na hivyo, sisi tumewaandikia barua TFF kuwaambia tunataka kujua, kwamba Simba imeonekana tumefoji mkataba, vipi imekuwa kimya? Watupe barua na maelezo kivipi.

“Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema angefuatilia hadi mwisho na jibu angetupatia. Vipi hadi sasa kimya?

“Kama itaendelea kuwa kimya hivi, tunaweza kuchukua hatua nyingine za kisheria, halafu tutaonekana kama sisi ni wakorofi, hatujafuata sheria za kimpira.

“Kama wao wapo kimya, sisi tutalipeleka polisi na mahakamani hilo suala. Tuwashitaki kwa mtu kufoji saini, jambo ambalo ni kinyume na sheria,” alisema Hans Poppe.


Wakati suala hilo likiendelea, kulikuwa na lawama za figisu kwamba Messi tayari alishafanya mazungumzo na Azam FC hata kabla ya kushinda kesi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic