October 16, 2015

KIBADENI

Baada ya kikosi cha JKT Ruvu kumkabidhi timu kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni ‘King’, imebainika ataifundisha timu hiyo bila kuwa na mkataba kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine.


Mara baada ya kukabidhiwa majukumu hayo, Kibadeni akaomba kocha msaidizi wa zamani wa Kagera Sugar, Mrage Kabange awe msaidizi wake, jambo ambalo halikupingwa, lakini kutokana na majukumu mengine yakiwemo ya kituo chake cha soka cha KISA (Kibadeni Soka Academy) kilichopo Chanika jijini Dar es Salaam, akaomba kutopewa mkataba ili kutojibana.

“Nimekubali kuisaidia timu, masuala ya fedha nimeweka kando ingawa sitakuwa na timu muda wote kutokana na kuwa na majukumu mengine. Ndiyo maana nilipoombwa kufanya kazi nikaomba niwe na Kabange kwa kuwa namjua vizuri utendaji wake,” alisema Kibadeni na kuongeza:


“Kuna muda (JKT Ruvu) watakuwa wanakuja kwenye academy yangu kufanya mazoezi, maana kuna wachezaji wenye vipaji na sitaki vipotee.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic