October 16, 2015


Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Mbeya City inatarajiwa kuikaribisha Simba, kesho Jumamosi katika Ligi Kuu Bara lakini ujio wa kiungo Haruna Moshi ‘Boban’ umeongeza nguvu kwenye kikosi cha Mbeya City ambapo amesema anaamini timu yake itaibuka na ushindi.


Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu yake hiyo, jana kwenye Uwanja wa Sokoine, Boban alisema kwa jinsi alivyowaona wenzake katika muda mfupi, anaamini ushindi utapatikana.

“Hii imekuwa siku nzuri kwangu, nimegundua timu yetu ina kikosi bora, vijana wana vipaji na uwezo mkubwa wa kucheza soka, binafsi hili limenishangaza na kunipa imani kuwa Simba hawana nafasi kwetu Jumamosi, tutawafunga,” alisema Boban.

Wakati huohuo, mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, umesababisha kuwe na gumzo kubwa mkoani hapa, ambapo umekuwa ukizungumzwa katika vijiwe vingi vya soka.

Kutokana na hali hiyo, ulinzi ulikuwa mkali katika mazoezi ya Mbeya City ambayo ipo chini ya Kocha Meja Abdul Mingange.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic