Kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Khamis
Mcha, amerejea rasmi uwanjani kuvaana na Yanga baada ya kuwa nje kwa miezi
kadhaa huku kiungo Michael Bolou, akitarajiwa kuanza mazoezi mepesi wiki mbili
zijazo.
Kiungo huyo ambaye pia anakipiga anakipiga katika timu yake ya taifa ya Zanzibar, alipata majeraha ya mguu
hata kabla ya michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika mapema mwezi Julai mpaka
Agosti, mwaka huu, baada ya kuvunjika mguu.
Daktari wa timu hiyo, Twalibu Misuli,
alisema kwa wachezaji waliopo kambini kwa sasa, wote wapo fiti hata Mcha ambaye
alikuwa nje, bado kidogo tu Bolou ambaye kwa sasa hawezi kucheza.
“Mcha kwa sasa yupo fiti, anaendelea na
mazoezi na timu kama kawaida, hata katika mchezo wa Yanga ni jukumu la kocha
kuweza kumtumia au kutomtumia lakini kiafya yupo vizuri kabisa.
“Lakini Bolou anatarajiwa kuanza mazoezi
mepesi wiki mbili zijazo baada ya kumaliza programu maalum ambayo alipewa ndani
ya mwezi mmoja, hivyo kwa sasa hakuna majeruhi wengine, zaidi tutawaangalia
afya zao hao ambao wanatoka timu ya taifa,” alisema Misuli.
0 COMMENTS:
Post a Comment