October 14, 2015


Simba imeendelea kufanya mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kuwawinda wenyeji Mbeya City katika mechi yao ya Jumamosi  katika muendelezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.


Mazoezi ya Simba ya jana yalikuwa kiboko kwani yalifanyika kwenye jua kali kuanzia saa saba na dakika nane mchana, hali ambayo iliwashtua mashabiki wengi.

Hata hivyo, wachezaji wa timu hiyo walionekana kuufurahia muda huo zaidi huku wakicheza na kutaniana kila mara.

Nyakati za asubuhi hapa Mbeya huwa na baridi kali ambayo kwa wachezaji waliotoka kwenye majiji ya joto kama Dar es Salaam hupata shida sana.

Hata hivyo burudani nyingine kwenye uwanja huo wa Sokoine ni kitendo cha kocha wa Simba, Dylan Kerr, kuungana na wachezaji wake kufanya mazoezi ambayo yalikuwa yakisimamiwa na Selemani Matola.


Kerr amekuwa akifanya hivyo mara nyingi akipambana na wachezaji wake ile kikwelikweli na si utani aseee.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic