MASHABIKI WA MBEYA CITY |
Uongozi wa Mbeya City, umeamua kuunda kamati maalum kuchunguza
suala la beki na nahodha wake, Juma Said Nyosso.
Uamuzi huo umetokana na Nyosso kubainika akimtendea udhalilishaji
nahodha wa Azam FC, John Bocco.
Taarifa zimeeleza, kamati hiyo itatoa majibu kesho kwa bodi ya jiji la Mbeya na baada ya hapo utaelezwa uamuzi hasa ni upi.
Tayari TFF imetoa adhabu kali ya miaka miwili kutocheza soka na
faini ya Sh milioni mbili kwa Nyosso.
Lakini ajabu, pamoja na kuonekana kwenye picha akifanya jambo
hilo, Nyosso ameanzisha kampeni za kukana jambo hilo.
Nyosso amekuwa akidai hakumbuki kufanya hivyo tena akinadai
teknolojia inaweza ikawa inamhukumu.
0 COMMENTS:
Post a Comment