Straika hatari wa Taifa Stars, Mbwana
Samatta anayekipiga katika timu ya TP Mazembe ya DR Congo ameahidi kufa na
Algeria kwa kuisaidia timu yake kufanya vizuri licha ya kukiri kuwa mchezo
utakuwa mgumu.
Stars inatarajia kukutana na Algeria Novemba 14, baada ya kuiondoa Malawi katika
mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa
kufanyika mwaka 2018 nchini Urusi huku mchezo wa marudiano ukichezwa Novemba
17.
Samatta akiwa Congo amesema kuwa,
wanatarajia kukutana na upinzani mkubwa katika mchezo huo hasa ukizingatia
wapinzani wao wapo vizuri na kudai kuwa yeye kama mchezaji wa kimataifa
amejipanga ipasavyo kukabiliana na wapinzani wao ili Stars iweze kusonga Mbele.
“Kwa upande wangu nimejipanga vizuri
kuhakikisha timu yangu inasonga mbele na kutoa mchango wangu mkubwa katika hii
mechi na nina mengi nitakayowashauri wezangu ili tuweze kushinda.
“Mechi itakuwa ngumu kwa upande wetu,
ukiangalia Algeria walivyo kwa sasa na timu yao inavyoundwa na wachezaji wengi
wenye viwango vizuri ni wazi mechi itakuwa na ushindani mkubwa.
“Kitu cha msingi tunachotakiwa kukifanya ni
kuhakikisha tunajipanga ili kuleta ushindani na kuweza kufanikiwa kufanya
vizuri katika mchezo huo kwa kujituma na kutokata tamaa,” alisema Samatta.
0 COMMENTS:
Post a Comment