October 28, 2015

LUHENDE WAKATI YANGA
Beki wa zamani wa Yanga, David Luhende, ambaye kwa sasa anaitumikia Mwadui FC ya Shinyanga, ameibuka na kusema wamejipanga vizuri kuwazuia washambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma, raia wa Zimbabwe na Mrundi, Amissi Tambwe.


Luhende ameyasema hayo wakati leo Jumatano wanatarajiwa kupambana na Yanga kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Luhende alisema tayari wamejipanga kuwazuia Yanga kuibuka na ushindi.

“Tumejipanga kuwazuia Yanga kushinda dhidi yetu, pia hao washambuliaji wao tunaamini tutawadhibiti ipasavyo wasilete madhara.


“Kikubwa tunaomba Mungu atuongoze salama kwani tunataka kuwa timu ya kwanza kuifunga Yanga msimu huu na hilo linawezekana kabisa kwa jinsi kila mmoja kikosini hapa alivyo na morali ya ushindi,” alisema Luhende.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic