Beki na nahodha wa Yanga
Nadir Haroub Cannvaro amefunguka kuwa anafurahi kuona Simba inavyoyumba kwa
sasa na wao wakizidi kuwaacha katika kuwania ubingwa na anaomba waendelee
kuyumba mpaka mwisho wa msimu.
Yanga kwa sasa inaongoza Ligi Kuu Bara kwa
pointi 19 sawa na Azam walio nafasi ya pili. Lakini Wanajangwani hao wapo juu
kwa tofauti ya mabao. Simba yenyewe ipo nafasi ya tano ikifungana na Stand
United iliyo nafasi ya nne kwa pointi 15.
Mpaka sasa Simba imefungwa michezo miwili na
kushinda mitano wakati mahasimu wao Yanga wamefanikiwa kusinda mechi sita na
kusuluhu mmoja mpaka sasa.
“Hiyo haina tatizo, kama Simba inafungwa na
kuporomoka ndiyo sawasawa maana tunazidi kuiacha na inakuwa afadhali kwetu,
tunapunguza watu tunaofukuzana nao huku juu, ikiendelea kufanya vibaya mpaka
mwisho wa msimu hiyo itakuwa na faida sana,” alisema Cannavaro.
Pamoja na hayo, taarifa zinaeleza zaidi kuwa
Simba sasa kunawaka moto kuhusiana na matokeo hayo na imeelezwa uongozi
umemkalia kooni kocha wao, Muingereza, Dylan Kerr na kwamba ajira yake ipo
mashakani.
0 COMMENTS:
Post a Comment