October 27, 2015


Licha ya Messi kuwa majeruhi, lakini Barcelona inaona ni vema kumuongezea mkataba mpya licha ya kwamba bado ana muda katika mkataba wake.


Mkataba wa Messi na Barcelona uliongezwa Mei 2014 na utaisha mwaka 2018.

Lakini uongozi wa Barcelona unaona unaweza kuongeza mkataba mpya na mkali huyo ambaye tayari ameshinda tuzo nne za Ballon d'Or.


Tayari mazungumzo ya awali yamefanyika na Messi amethibitisha anataka kuendelea kubaki Barcelona.

Hata hivyo bado haijajulikana mkataba huo utakuwa ni wa muda gani na Messi ataongezewa kiasi gani kwani katika mkataba wa sasa baada ya kukatwa kodi kwa mwaka, Messi analamba euro milioni 20.


1 COMMENTS:

  1. Messi s'est établi parmi les meilleurs joueurs du monde avant l'âge de 20 ans.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic