MOJA YA NDEGE ZA FAST JET. |
Timu ya soka ya taifa 'Taifa Stars', inatarajiwa kusafiri na ndege ya binafsi ya kukodi
ya shirika la Fastjet kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano
utakaochezwa Novemba 17 mjini Algiers.
MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA STARS, FAROUKH BAGHOZA |
Jimmy amesema
katika safari hiyo, Fastjet itatoa ndege yenye uwezo wa kubeba abiria 156
walioketi, sambamba na wafanyakazi wa ndenge, ambapo wao wametoa punguzo la
asilimia 35 katika gharama nzima ya safari ya kuelekea Algeria.
Aidha, Jimmy
ameongeza kuwa safari hiyo itakua ni ya masaa 7 ambapo ndege ikitoka Dar es
salaam itatua Djamena – Chad kuongeza mafuta kabla ya kuendelea tena na safari
mpaka nchini Algeria.
Naye katibu wa
kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda aliwashukuru Fastjet kwa kukubali kuwa
wasafirishaji rasmi wa TaifA Stars kwa mechi dhidi ya Algeria, huku akisema
gharama za safari za mtu mmoja kusafiri ni dolla 800 kwenda na kurudi.
Teddy amewaomba
watanzania, wapenzi, washabiki wa mpira wa miguu wanaotaka kusafiri kufika
ofisi za TFF zilizopo Karume kwa ajili ya kujiandiksha na kuelekea taratibu nzima
za safari.
0 COMMENTS:
Post a Comment