Beki mkongwe wa Majimaji FC ya Songea, Fredi Mbuna,
amefunguka kuwa licha ya kupokea kipigo cha mabao 6-1 dhidi ya Simba, kamwe
hawawezi kushuka daraja kutokana na kipigo hicho.
Nahodha huyo wa zamani wa Yanga na sasa Majimaji, ni
miongoni mwa wachezaji walioipandisha timu hiyo katika Ligi Kuu Bara na
ameyaeleza hayo kutokana na kichapo kilichoanza kuzua hofu klabuni hapo.
Mbuna alisema kuwa
kupoteza mchezo huo siyo sababu itakayowafanya washuke daraja.
“Kiukweli tumepoteza kwa idadi kubwa ya mabao,
hatukutarajia kufungwa kwa idadi ile lakini haimaanishi kuwa sasa tutashuka.
“Sasa tutakachofanya ni kujituma zaidi ili tuweze
kufanya vizuri kwenye michezo inayokuja huko mbele,” alisema Mbuna.
0 COMMENTS:
Post a Comment